MAJAMBAZI WAUA MMOJA KATAVI,WAJERUHI WENGINE NA KUPORA FEDHA
Na.Issack Gerald Mtu mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Hassan Damsoni mkazi wa kijiji cha Katambike kata ya Ugalla Mkoani Katavi ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi. Kwa mjibu wa diwani wa kata hiyo Mh.Halawa Malembeja amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano usiku ambapo mbali na kuuwawa kwa makzi huyo watu hao wamepora zaidi ya shilingi milioni mbili kutoka nyumba tano na kujeruhi wengine. Kwa mjibu wa Diwani Malembeja mazishi ya marehemu yamekwishafanyika katika kijiji hicho huku akieleza kuwa wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuliomba jeshi la polisi kupeleka kituo cha polisi katika kata hiyo kwa ajili ya usalama. Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesema wamemkamata mtu mmoja akiwa na silaha aina ya gobole na simu tano ambazo zilikuwa zimeondolewa. Hata hiyo Jeshi la polisi limetoa wito kwa watu kuacha kujihusisha na uharifu kwani kufanya hivyo ni ...