DIWANI ATAKA MKURUGENZI ATAFUTE MAENEO KWA AJILI YA WAPIGA KURA WAKE
Diwani wa Kata ya Mpanda Hotel
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Willium Liwali amemshauri Mkurugenzi
mtendaji Manispaa ya Mpanda kutafuta mahali pa kuwaweka wafanyabiashara wadodo
wadogo wapatao 200 wa kata hiyo waliokosa nafasi ya kufanyia biashara.
Mh.Liwali amesema hayo kufuatia agizo
la Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu kuagiza wafanyabiashara wote
walio katika masoko yasiyo rasmi katika Manispaa hiyo kutakiwa kuondoka na
kufanyia biashara zao katika masoko rasmi.
Kwa mjibu wa Diwani Liwali masoko
yote ambayo wafanyabiashara hao wangehamia yakiwemo soko la Mpanda Hotel
lililopo kata ya Majengo na soko la Kachoma lililopo kata ya Makanyagio yote
yamejaa.
Wiki iliyopita,mamia ya
wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanyia biashara zao katika machinjio ya
ng’ombe Mpanda Hotel waliandamana mpaka kituo cha Radio Mpanda Fm wakipinga
agizo la Mkurugenzi anayewataka kuondoka katika maeneo hayo yasiyo rasmi.
Kwa mjibu wa agizo la Mkurugenzi
Michael Nzyungu,wafanyabiashara wote walio katika maeneo yasiyo halali kwa
biashara walitakiwa wawe wameondoka mpaka kufikia Januari 22 mwaka huu suala
ambalo mpaka sasa limeshindikana.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments