ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBC AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTAPANYA SHILINGI MIL. 897
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la
Utangazaji Tanzania TBC, Tido Mhando amefikishwa mahakamani jijini Dar es
Salaam kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka.
Tido Mhando |
Tido Mhando,ambaye kwa sasa ni
Mkurugenzi wa Azam Media alifikishwa katika mahakama ya Kisutu mapema jana
Ijumaa na kusomewa dhidi mashtaka yake.
Wakili wa Taasisi ya Kupambana na
Rushwa Tanzania (Takukuru) Leonard Swai alimwaambia hakimu mkazi mkuu Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka
matano.
Bw.Mhando anadaiwa kutenda makosa
hayo mwaka 2008 alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC na anatuhumiwa kwa matumizi
mabaya ya madaraka wakati alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la
Serikali TBC ambapo anadaiwa kulitia hasara taifa shilingi milioni 897.
Hata hivyo Mhando amekana mashtaka
yote na kuachiwa kwa dhamana ambapo kesi imeahirishwa hadi Februari 23mwaka huu
kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Sheria nchini Tanzania haiwaruhusu
washtakiwa,mawakili au watu wengine kuzungumzia kesi nje ya mahakama.
Mhando ni miongoni mwa waandishi wa
habari na watangazaji wakongwe wa Tanzania na aliwahi kufanya kazi Shirika la
Utangazaji Uingereza (BBC) kama Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili kabla ya kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa TBC.
Pia amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya
Mwananchi,Mwanspoti na The Citizen.
Katika hatua nyingine aliwahi
kufanyia kazi Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle),Sauti ya Amerika na Shirika
la Utangazaji la Kenya (KBC) lilipokuwa linafahamika kama Sauti ya Kenya (VoK).
Chanzo:bbc
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments