WAWILI WAUWAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI KATAVI
Na.Issack Gerald
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi
limewauwa watu wawili kati ya watano waliokuwa na silaha tatu za kivita aina ya
SMG ambapo watu hao wameuawa wakati wa majibizano kati yao na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP
Damasi Nyanda amesema tukio hilo limetokea Januari 25 mwaka huu katika kijiji
cha Kapalamsenga Wilayani Tanganyika ambapo watu hao wamekutwa wakiwa na risasi
16 na Magazini 5.
Aidha Kamanda Nyanda amesema watu hao
wamekutwa na meno ya Tembo yenye uzito wa kilo 6.6 yakiwa na thamani ya zaidi
ya Shilingi milioni 34 pamoja na nyama
ya pofu kilo 20 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3
Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya taifa
ya Katavi Zumbe Msindai amesema kukamatwa kwa watu hao kumetokana na
ushirikiano kati yao na jeshi Polisi Mkoani Katavi ikiwa ni baada ya kupata
taarifa za siri juu ya uwepo wa watu hao.
Watuhumiwa wote wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments