MAJAMBAZI WAUA MMOJA KATAVI,WAJERUHI WENGINE NA KUPORA FEDHA
Na.Issack Gerald
Mtu mmoja aliyekuwa akijulikana kwa
jina la Hassan Damsoni mkazi wa kijiji cha Katambike kata ya Ugalla Mkoani Katavi
ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Kwa mjibu wa diwani wa kata hiyo Mh.Halawa
Malembeja amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa
tano usiku ambapo mbali na kuuwawa kwa makzi huyo watu hao wamepora zaidi ya
shilingi milioni mbili kutoka nyumba tano na kujeruhi wengine.
Kwa mjibu wa Diwani Malembeja mazishi
ya marehemu yamekwishafanyika katika kijiji hicho huku akieleza kuwa wananchi
wamesikitishwa na tukio hilo na kuliomba jeshi la polisi kupeleka kituo cha
polisi katika kata hiyo kwa ajili ya usalama.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi
Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesema
wamemkamata mtu mmoja akiwa na silaha aina ya gobole na simu tano ambazo
zilikuwa zimeondolewa.
Hata hiyo Jeshi la polisi limetoa
wito kwa watu kuacha kujihusisha na uharifu kwani kufanya hivyo ni kosa
kisheria ambapo msako unaendelea ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo ili
wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Hilo ni tukio la pili kwa mtu kuuwawa
katika kipindi cha wiki moja baada ya tukio la kifo cha mwanafunzi wa darasa la
sita kuuwawa na watu wasiojulikana wilayani Tanganyika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments