WAZIRI AAGIZA WALIONYANG’ANYWA PIKIPIKI NA POLISI KURUDISHIWA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani,Dkt.Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo. Dkt.Nchema amesema waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu. Dkt.Mwigulu amesema zile zenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita,madawa ya kulevya na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakamani au kuziteketeza huku akisema zenye makosa madogo wazitatue haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.