MAGAIDI WAWILI HATARI WA IS WAKAMATWA
Raia wawili wa Uingereza
wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislam cha IS
wanashikiliwa na kundi la wapigaji wa Kikurd.
Alexanda Kotey(34) na mwenzake El Shafee
Elsheikh(29) ni miongoni mwa vijana wawili waliokuwa wanasakwa kati ya wenzao
ambao walikwisha kukamatwa.
Kundi
hili la vijana wanne kutoka raia wa Uingereza ndani ya kundi la IS walikuwa ni
kundi hatari linalofahamika kama Beatles hiyo ikiwa ni kutokana na lafudhi yao
wanapozungumza.
Maofisa
wa Marekani wamesema kundi hilo lililokuwa likihusika na utoaji mateso pamoja
na kuua ndani ya IS linadaiwa kuwachinja Zaidi ya watu 27 mateka kutoka nchi za
kimagharibi na kutoa mateso makali kwa wengine wengi tu.
Hawa ni kundi hatari kwa ajili ya mauaji
na mateso,ambalo lilikuwa linajumuisha watu kama Mohammed Emwazi almaarufu kama
Jihadi John ambaye alikuwa akionekana katika picha za video akiwa anachinja
watu.
Aliuawa katika mashambulizi ya anga mwaka
2015 katika mji wa Raqqa ngome ya zamani ya IS.
Lakini
wapo pia Aine Davis ambaye naye alikuwa akitokea Uingereza,alihukumiwa baada ya
kubainika kuwa alikuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa kundi la Islamic State
na alifungwa mwaka jana huko Uturuki.
Wengine wanaounda kundi hili la Beatles
ni Alexanda Kotey ambaye naye anatoka London magharibi ambapo kwa mjibu wa
Marekani yeye alikuwa katika kitengo cha utesaji na alikuwa mtu anayetoa
usajili kwa wanaojiunga na IS.
El
Shafee Elsheikh huyu yeye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda genge hili hawa
ndiyo Beatles.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments