WAZIRI AAGIZA WALIONYANG’ANYWA PIKIPIKI NA POLISI KURUDISHIWA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani,Dkt.Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la
polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina
makosa madogo.
Dkt.Nchema amesema waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka
zikawa vyuma chakavu.
Dkt.Mwigulu amesema zile zenye makosa makubwa kama uhalifu wa
kivita,madawa ya kulevya na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu
wa kuwapeleka mahakamani au kuziteketeza huku akisema zenye makosa madogo
wazitatue haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.
Alisema ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria
ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki
katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita vituo vya polisi hukuta
pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments