AJALI YA TRENI KATAVI
Mabehewa 4 ya Treni ya mizigo ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Wilayani Mpanda Mkoani Mpanda Katavi kuelekea Tabora yameacha njia na kuanguka. Afisa Uhusiano Shirika la Reli Mohamed Mapondela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema mabehewa hayo yameangukia katika eneo la Shankala mkoani Katavi. Amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala uharibifu wa mali na kinachoendelea kwa sasa kutoa mizigo na kuweka sawa njia ya treni ili kuruhusu safari ziendelee kama kawaida. Kwa upande mwingine Bw.Mapondela hakueleza sababu hasa zilizosababisha ajali hiyo kutokea lakini amesema huenda ikawa imechangiwa na uchakavu wa njia hiyo ya treni. Reli hiyo inayotajwa kuwa ni miongoni mwa reli kongwe zilizojengwa nchini enzi za ukoloni miongo kadhaa iliyopita. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com