AJALI YA TRENI KATAVI
Mabehewa 4 ya Treni ya mizigo ambayo
ilikuwa ikisafiri kutoka Wilayani Mpanda Mkoani Mpanda Katavi kuelekea Tabora
yameacha njia na kuanguka.
Afisa Uhusiano Shirika la
Reli Mohamed Mapondela amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema mabehewa hayo yameangukia katika eneo la
Shankala mkoani Katavi.
Amesema hakuna mtu
aliyejeruhiwa wala uharibifu wa mali na kinachoendelea kwa sasa kutoa mizigo na
kuweka sawa njia ya treni ili kuruhusu safari ziendelee kama kawaida.
Kwa upande mwingine Bw.Mapondela
hakueleza sababu hasa zilizosababisha ajali hiyo kutokea lakini amesema huenda ikawa imechangiwa na uchakavu wa njia hiyo ya
treni.
Reli hiyo inayotajwa kuwa ni
miongoni mwa reli kongwe zilizojengwa nchini enzi za ukoloni miongo kadhaa
iliyopita.
Comments