Posts

Showing posts from February 7, 2018

JAJI MKUU WA KENYA AILAUMU SERIKALI YAKE KUKIUKA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI

Image
Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha sheria na katiba ya kenya katika kukabiliana na upinzani. Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga Tamko hilo limekuja mara tu baada ya kiongozi mmoja wa upinzani wakili Miguna Miguna kufukuziwa nchini Canada,baada ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano hata baada ya mahakama kutoa amri kwamba aachiliwe kwa dhamana . Katika maelezo yake jaji David Maraga,amesema malalamiko yaliyopelewekwa mahakamani yalikuwa wazi,na yalikuwa majukumu ya mahakama kufanya maamuzi kwa kuwa ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe. Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama. Kwa mjibu wa madai ya serikali ya Kenya ni Kwamba Miguna Miguna alishakana uraia wa Kenya na kuchukua uraia wa Canada ambapo kata hivyo kwa mjibu wa katiba ya Kenya raia wan chi hiyo anaruhu...

HABARI PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA FEBRUARI 7,2018

Image
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kutekeleza dhana ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjelina Mabula akisisistiza umuhimu wa Halmashauri kutenga maeneo ambayo yatatumiwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kujenga nyumba za gharama nafuu zitakazouzwa kwa wananchi na watumishi wa Halamshauri husika. Mbunge wa Urambo Mashariki Mhe. Magreth Sita akiuliza Swali Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutatua migogoro ya Ardhi ikiwemo kubatilisha matumizi ya mashamba ambayo hayajaendelezwa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Aderladus Kilangi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati hiyo kwa...

SERIKALI KUENDELEA KUWEKA ALAMA YA MIPAKA YA HIFADHI NA MAKAZI

Image
Serikali imesema itaendelea kuweka alama za mipaka ya hifadhi mbalimbali hapa nchini pamoja na kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa mistu ili kuepusha migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Maliasili na utalii Josephati Hasunga wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mkoani Tabora Magreth Simwanza Sitta aliyekuwa akihoji kuhusu mpango wa serikali kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya msitu wa North Ugalla na wanaozunguka msitu huo. Akijibu swali la nyongeza la Mh.Sitta pamoja na mambo mengine Mh.Hasunga amesema mara baada ya mkutano wa bunge wataalamu watapanga ratiba ili kufika kwa mara nying8ine Mkoani Tabora ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya mipaka iliyopo kati ya wananchi na hifadhi. Kwa mjibu wa Mh.Hasunga Misitu ya hifadhi ya Norh Ugalla ina ushoroba wa wanayama ambao mara nyingi husafriri mpaka Hifadhi ya taifa ya Wanyama ya Katavi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

ASKARI MAGEREZA 11 WASIMAMISHWA KAZI

Image
Jeshi la Magereza Tanzania limewasimamisha kazi askari wake 11 waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Aloyce Makalla (41) mkazi wa Kijiji cha Kerenge wiki iliyopita. Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zinaeleza kuwa askari hao walisimamishwa kazi na Kamishna Jenerali wa Magereza,Dk Juma Malewa juzi. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga,John Masunga alithibitisha kusimamishwa kwa askari hao lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi akisisitiza kuwa msemaji wa jeshi hilo ni Kamishna Jenerali pekee. Askari waliosimamishwa ambao walishafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Korogwe mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kassim Mkwawa ni Jonas Makere,Shadrack Lugendo,Lazaro Stephen,Mussa Zuberi,Ramadhan Yusuf,Robert Alfred,Fhidirish Osmas,Alfonce Revocatus,Mbesha Naftari,Hamis Msola na Michael Elias.

TMA YATOA ANGALIZO

Image
Mamlaka ya hali ya hewa nchini imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa mvua kubwa katika baadhi ya mikoa ya Rukwa, Mbeya,Songwe,Iringa,Njombe na Ruvuma kuanzia leo usiku. Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa. Aidha taarifa hiyo inaonesha mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam,Pwani,Lindi,Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Mamlaka ya hali ya hewa ipo chini ya Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano hapa nchini.

TETESI ZA SOKA ULAYA NA AFRIKA MASHARIKI JUMATANO 07.02.2018

Image
  Mkufunzi wa Cheslea Antonio Conte Aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Luis Enrique ni miongoni mwa makocha walioorodheshwa na mmiliki wa timu hiyo Roman Abrahamovic kuchukua mahala pake mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte iwapo atafutwa kazi. (Sport - in Spanish) Enrique ambaye ni raia wa Uhispania inadaiwa atamsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez iwapo atasajiliwa kuifunza The Blues. (Le10Sport - in French) Mechi kali inatarajiwa kati ya Njombe Mji na Young Africans katika uwanja wa Uhuru . Mchezo wa Yanga umeimarika pakubwa katika siku za hivi karibuni. Walisitisha matumaini ya klabu ya Azam ya kukamilisha msimu mzima bila kupoteza mechi wakiwashinda 2-1 katika uwanja wa Azam katika mechi mbili za mwisho ilizocheza.{The Citizen Tanzania}. Hatahivyo, Enrique hayuko tayari kukatiza likizo yake kutoka katika soka na kwamba yuko tayari kuchukua kazi hiyo mwisho wa msimu huu.(Goal). Aliyekuwa kocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique ...

BEI MPYA YA MAFUTA INAYOANZA KOTE KUTUMIKA NCHINI

Image
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo Februari 7 huku bei za petroli,dizeli na mafuta ya taa zikipanda. Taarifa ambayo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Nzinyangwa Mchany amesema bei za rejareja zimeongezeka kwa petroli ikiwa ni Sh59 sawa na 2.70%,dizeli Sh46 sawa na 2.30%,na mafuta ya taa kwa Sh24 sawa na 1.17%. Wakati huo huo amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambao kwa petroli ni Shilingi 58.57 sawa na 2.85%,dizeli kwa Shilingi 46.48 sawa na 2.44% na mafuta ya taa kwa Shilingi 23.75 sawa na 1.24%. Mchany amesema ongezeko hilo linatokana na bei kuongezeka katika soko la dunia.

KENYA YAZUNGUMZIA UAMUZI WA KUMFUKUZA MIGUNA

Image
Wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya imesema wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna alipata hati ya kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake. Jana usiku mamlaka nchini Kenya zilimfukuza ghafla Miguna na kumpandisha katika ndege ya shirika la Uholanzi la KLM kuelekea nchini Canada. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa huku wengi wakiilaani serikali ya Kenya kuwa ilikiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo na haki za kiraia za bwana Miguna Katika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009. Miguna alifukuzwa nchini Kenya mara baada ya kushiriki katika kiapo kisicho rasmi cha Raila Odinga kuwa rais wa watu wa Kenya mwezi uliopita. Odinga ni mwanasiasa wa upinzani ambaye alisusia marudio...

DC AKABIDHI GARI LA KUZOA TAKA

Image
MKUU wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi.Lilian Charles Matinga,amekabidhi lori jipya la kuzoa taka katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda. Bi.Matinga mbali na kuwapongeza Halmashauri kwa kununua gari hilo,ametaka gari hilo litumike kwa ajili ya kufanya usafi kwa kuzoa taka kama lilivyokusudiwa. Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Wilium Mbogo mara baada ya kukabidhiwa gari hilo,amesema gari hilo limetokana na fedha ambazo zilikuwa zimepangwa kutumika kununua gari la la Meya ambapo amewapongeza baraza la madiwani kwa kubadili matumizi hayo kwa ajili ya maslahi ya Halmashauri. Naye Kaimu mkuruingenzi wa Manispaa ya Mpanda Deodatus Kangu, amesema shilingi milioni 159 zilizotumika kununua gari hilo zimetokana na makusanyo ya ndani ya manispaa na amesema kuwa litasaidia kuzoa taka kwa wakati.

CUF YA MAALIM SEIF YAJIPANGA KUKABILI NJAMA ZA LIPUMBA

Image
Naibu Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kwa upande wa Maalim Seif,Mbarala Maharagande amesema Profesa Lipumba pamoja na genge lake wamepanga njama za kuwafukuza madiwani wote wa CUF Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari,Maharagande amesema Lipumba amepanga njama za kuwafukuza madiwani wa CUF Dar es Salaam wakiwepo wastahiki Meya kutokana na madiwani hao kutokuwa na ushirikiano na Lipumba pamoja na kundi lake. Hata hivyo Maharagande amedai chama hicho kimejipanga vyema kukabiliana na njama hizo zinazotaka kufanywa na Profesa Ibrahim Lipumba. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

KIONGOZI NRM KENYA APANDISHWA NDEGE KWA LAZIMA KUTOKA KENYA MPAKA KANADA AKIHUSISHWA NA KIAPO CHA RAILA

Image
Mwanasiasa wa muungano wa upinzani nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna amefukuzwa na kupelekwa nchini Canada kupitia ndege ya KLM. Serikali yamfurusha Miguna Miguna na kumpeleka Canada Kwa mjibu wa mawakili wa Miguna Nelson Havi na Cliff Ombeta Ombeta waliarifiwa kuwa Bw.Miguna aliingizwa katika ndege iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada huku wakili mwingine Dkt.John Khaminwa akisema mteja wake tayari ameondoka Kenya. Haijulikani ni sheria gani iliyotumiwa na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo. Kwa mjibu wa mawaikili hao,wakati Miguna alipokamatwa serikali ya Canada ilikuwa imeiandikia Kenya kionyesha wasiwasi kwamba raia wake alikuwa ananyanyaswa na walitaka arudishwe nchini humo. Siku ya jana Bw.Miguna alisema alikamatwa bila mawasiliano na familia yake ama wakili wake kwa siku tano akisema kuwa kuwa maafisa wa polisi walimnyanyasa kwa kumfungia katika maeneo ambayo hayafai ...