CUF YA MAALIM SEIF YAJIPANGA KUKABILI NJAMA ZA LIPUMBA
Naibu Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na
Mahusiano na Umma wa CUF kwa upande wa Maalim Seif,Mbarala Maharagande amesema
Profesa Lipumba pamoja na genge lake wamepanga njama za kuwafukuza madiwani
wote wa CUF Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari,Maharagande
amesema Lipumba amepanga njama za kuwafukuza madiwani wa CUF Dar es Salaam
wakiwepo wastahiki Meya kutokana na madiwani hao kutokuwa na ushirikiano na
Lipumba pamoja na kundi lake.
Hata hivyo Maharagande amedai chama
hicho kimejipanga vyema kukabiliana na njama hizo zinazotaka kufanywa na Profesa
Ibrahim Lipumba.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments