KIONGOZI NRM KENYA APANDISHWA NDEGE KWA LAZIMA KUTOKA KENYA MPAKA KANADA AKIHUSISHWA NA KIAPO CHA RAILA
Mwanasiasa wa muungano wa upinzani
nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna amefukuzwa na kupelekwa nchini Canada kupitia
ndege ya KLM.
Serikali yamfurusha Miguna Miguna na kumpeleka Canada |
Kwa mjibu wa mawakili wa Miguna Nelson
Havi na Cliff Ombeta Ombeta waliarifiwa kuwa Bw.Miguna aliingizwa katika ndege
iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada huku wakili mwingine
Dkt.John Khaminwa akisema mteja wake tayari ameondoka Kenya.
Haijulikani ni sheria gani iliyotumiwa
na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba inampatia haki kama raia wa
Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo.
Kwa mjibu wa mawaikili hao,wakati
Miguna alipokamatwa serikali ya Canada ilikuwa imeiandikia Kenya kionyesha
wasiwasi kwamba raia wake alikuwa ananyanyaswa na walitaka arudishwe nchini
humo.
Siku ya jana Bw.Miguna alisema
alikamatwa bila mawasiliano na familia yake ama wakili wake kwa siku tano
akisema kuwa kuwa maafisa wa polisi walimnyanyasa kwa kumfungia katika maeneo
ambayo hayafai kwa binaadamu.
Ripoti za kufurushwa nchini Kenya
zilijiri saa chache baada ya jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru kumzuia
mkurugenzi wa Ujasusi na inspekta jenerali wa polisi dhidi ya kumwekea mashtaka
yoyote.
Jaji huyo awali alikuwa ameamuru
kwamba inspekta jenerali wa polisi na mkurugenzi wa shirika la ujasusi walikuwa
wamekiuka agizo la mahakama lililowataka kumwachilia kiongozi huyo.
Huku Jaji huyo wa Kajiado akiagiza
awasilishwe mbele ya jaji Kimaru katika mahakama ya Milimani,bwana Miguna
hakuwasilishwa katika mahakama hiyo huku mawakili wake wakilazimika kusubiri
hadi usiku wakisubiri kuachiliwa kwake.
Miguna alikamatwa Ijumaa iliopita
huku jaji wa mahakama kuu James Wakiaga akimwachilia kwa dhamana ya ksh. 50,000
lakini hakuachiliwa.
Mkurugenzi wa shirika la ujasusi
baadaye alisema kuwa bwana Miguna alikamatwa baada ya kukiri kumpatia kiapo
kiongozi wa Nasa Raila Odinga mbali na kuwa mwanachama wa kundi lililopigwa
marufuku la NRM.
Mgiuna alikamatwa siku ya Ijumaa kwa
tuhuma za kushiriki katika sherehe ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila
Odinga ambaye aliapishwa kuwa rais wa wawananchi Januari 30 mwaka huu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments