SERIKALI KUENDELEA KUWEKA ALAMA YA MIPAKA YA HIFADHI NA MAKAZI


Serikali imesema itaendelea kuweka alama za mipaka ya hifadhi mbalimbali hapa nchini pamoja na kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa mistu ili kuepusha migogoro ya ardhi.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Maliasili na utalii Josephati Hasunga wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mkoani Tabora Magreth Simwanza Sitta aliyekuwa akihoji kuhusu mpango wa serikali kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya msitu wa North Ugalla na wanaozunguka msitu huo.
Akijibu swali la nyongeza la Mh.Sitta pamoja na mambo mengine Mh.Hasunga amesema mara baada ya mkutano wa bunge wataalamu watapanga ratiba ili kufika kwa mara nying8ine Mkoani Tabora ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya mipaka iliyopo kati ya wananchi na hifadhi.
Kwa mjibu wa Mh.Hasunga Misitu ya hifadhi ya Norh Ugalla ina ushoroba wa wanayama ambao mara nyingi husafriri mpaka Hifadhi ya taifa ya Wanyama ya Katavi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA