TETESI ZA SOKA ULAYA NA AFRIKA MASHARIKI JUMATANO 07.02.2018
Aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Luis Enrique ni miongoni mwa makocha walioorodheshwa na mmiliki wa timu hiyo Roman Abrahamovic kuchukua mahala pake mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte iwapo atafutwa kazi. (Sport - in Spanish)
Enrique
ambaye ni raia wa Uhispania inadaiwa atamsajili mshambuliaji wa
Barcelona Luis Suarez iwapo atasajiliwa kuifunza The Blues. (Le10Sport -
in French)
Mechi kali inatarajiwa kati ya Njombe Mji na Young
Africans katika uwanja wa Uhuru . Mchezo wa Yanga umeimarika pakubwa
katika siku za hivi karibuni. Walisitisha matumaini ya klabu ya Azam ya
kukamilisha msimu mzima bila kupoteza mechi wakiwashinda 2-1 katika
uwanja wa Azam katika mechi mbili za mwisho ilizocheza.{The Citizen
Tanzania}.
Hatahivyo, Enrique hayuko tayari kukatiza likizo yake
kutoka katika soka na kwamba yuko tayari kuchukua kazi hiyo mwisho wa
msimu huu.(Goal).
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte analipia makosa
yaliofanywa na mkurugenzi wa zamani wa kiufundi katika klabu hiyo
Michael Emenalo katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu uliopita
kulingana na mchezaji wa zamani na naibu mkufunzi Ray Wilkins.
(talksport)
Conte amesalia na miezi 18 katika kandarasi yake na kwamba hatowacha kazi (Mirror).
Abramovich hatoruhusu wachezaji kuamua iwapo Conte anfaa kusalia katika uwanja wa Stamford Bridge. (Telegraph)
Mabingwa
wa zamani wa ligi nchini Kenya AFC Leopards wanaelekea mjini Kakamega
siku ya Jumatano ili kujiandaa tayari kwa mechi yake ya kombe la Caf .
Mabingwa
hao wa kombe la Gotv wataikaribisha nyumbani klabu ya Madagascar Fosa
juniors katika awamu ya kwanza katika uwanj wa Bukhungu siku ya
Jumapili.Awamu ya pili ya mechi ya marudiano inatarajiwa kufanyika wiki
moja baadaye nchini Madagascar.{Nation Daily Newspaper}.
Kipa wa Chelsea na Ubelgiji Thibaut Courtois, 25,
anasema hali yake huenda ikamruhusu kuelekea klabu ya Real Madrid iwapo
mabingwa hao wa Ulaya wataonyessha hamu ya kutaka kumsajili. (Sport
Foot Magazine, via Daily Mail)
Kipa wa Manchester United David de
Gea atasalia kuwa kivutio kwa Real Madrid' katika dirisha la uhamisho la
mwisho wa msimu huu, lakini United inatarajiwa kumpatia raia huyo wa
Uhispania mkataba mpya. (Sport - in Spanish).
Wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda Cranes, Isaac Isinde na
Boban Zirintusa wameachiliwa na klabu ya Zambia Buildcon FC. Isinde na
Zirintusa ni miongoni mwa wachezaji 16 ambao klabu hiyo imewatoa.{New
Vision Uganda}.
Arsenal wana hamu ya kumsajili beki wa Juventus
Daniele Rugani, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo wa miaka 23 kutoka
Itali. (Star)
Liverpool Itamtoa kwa mkopo beki wa Colombia mwenye
umri wa miaka 18 Anderson Arroyo kwenda Real Mallorca baada ya kupokea
nakala za kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Fortaleza CEIF.
(Liverpool Echo).
Kipa wa Roma Alisson, anayelengwa na Liverpool, ni kipa bora
zaidi duniani na raia huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 ana thamani
ya Yuro 50m kulingana na kocha Roberto Negrsolo. (Il Romanista, via
Goal).
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Bolton,
Sunderland, Blackburn na Leeds El Hadji Diouf, 37, anataka kuwa
mwanasiasa nchini Senegel.(FourFourTwo)
Klabu ya Benevento, ambayo
iko pointi tisa chini ya ligi ya Serie A , imefanya majaribio ya
kuwasajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Samir Nasri na Alex Song,
wote wakiwa na umri wa 30, na wako huru. (Sky Italia - in Italian)
Comments