Posts

Showing posts from November 1, 2017

TFS WAMETOA ONYO KWA WAVAMIZI WA HIFADHI ZA MISITU MKOANI KATAVI

Image
Wakazi mkoani katavi wametakiwa kuacha tabia ya kuvamia misitu na kufanya shughuli katika hifadhi zinazoharibu uoto wa asili. Kauli hiyo imetolewa na Samwel Matula ambaye meneja wa misitu (TFS) kanda maalum ya mkoa wa Katavi ambapo amesema hakuna ruhusa ya watu kufanya shughuli kama kilimo au kuweka makazi katika hifadhi zilizopo katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo meneja misitu wilaya ya mpanda Mustafa Abedi amewataka wote walioondolewa katika maeneo ya misitu kufuatia operesheni iliyofanyika mwezi wa saba mwaka huu ,kutorudi katika maeneo hayo na sheria kali zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo. Mwezi Julai mwaka huu,operesheni ya kuwaondoa watu katika maeneo ya misitu kama vile msitu wa msaginya ,na misitu north east mpanda ilifanyika kwa lengo la kulinda misitu iliyopo Katavi kwa manufaa ya wananchi wote. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

MASOKO YA USIKU MKOANI KIGOMA,HOFU USALAMA IMETANDA

Imeelezwa kuwa Masoko ya usiku katika baadhi ya kata za wilaya ya Buhigwe mkoani kigoma,yanapalekea matatizo kwa wakazi wa wilaya hiyo,yakiwemo matatizo ya kiusalama kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi jirani ya Burundi. Diwani wa kata ya Mkatanga ambaye ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe,Bw.Hamiss Lukanka  amesema soko hasa lililoko katika kata ya Mkatanga linapelekea hata watoto wa shule kutokupata muda wa kujisomea kutokana kutumia muda wao mwingi hasa wa usiku kuzurula sokoni humo. Amesema mpaka sasa wana mpango wa kuratibu na kusimamia soko hilo liwe linaanza muda wa asubuhi kwa siku maalum,ili kuondokana na changamoto zinazotokana na masoko ya usiku na kutoa nafasi kwa wakazi wa vijiji jirani kuleta bidhaa zao katika soko hilo. Katika upande mwingine Bw.Lukanka amewataka wananchi wa wilaya ya Buhigwe kufanya kazi kwa kushilikiana Bila kujali utofauti wa vyama wilayani humo,lengo kubwa  likiwa ni kuleta maendeleo ya wilaya yao. Ch...

TIMU YA CCBRT SASA NI MKOANI KIGOMA

Image
  Kampeni ya uhamasishaji wa matibabu ya ugonjwa wa   fistula inayoendeshwa na CCBRT inayofanyika Tanzania nzima,hivi sasa timu ya uhamasishaji matibabu ya ugonjwa huo mkoani Kigoma. Akiongea na timu hiyo mkuu wa mkoa wa Kigoma Bregedia mstaafu Emanueli Maganga ameeleza kufurahishwa kwake na juhudi zinazofanywa na CCBRT na kubariki ujio wa timu hiyo kwani utasaidia katika kueneza elimu juu ya ugonjwa huo kwa wakazi wa kigoma. Kwa upande wake meneja wa mradi wa fistula kutoka hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es salaam Bwana Clement Ndahana amesema kuwa kwa kila mwaka zaidi ya akina mama 3000 nchini hupata ugonjwa wa fistula lakini akina mama 1400 ndio ambao hupata matibabu ya ugonjwa huo. Mara baada ya salamu mkoani humo timu hiyo ya uhamasishaji imeelekea wilayani uvinza kijiji cha Kalia kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika ambako wataanza  na uhamasishaji wa matibabu ya ugonjwa wa fistula mkoni humo. Chanzo:Isaac Isaac,Mhariri-Issack Gerald Haba...

VYOMBO VYA USAFIRI KUFANYIWA UKAGUZI

Image
Wamiliki na madereva wa vyombo vya moto Mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinafanyiwa ukaguzi. Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani Mkoani Katavi Nassoro Alphi ambapo amesema zoezi hilo linafanyika nchi nzima na litadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesema kuwa kwa mkoa wa katavi wameanza na magari ya abiria pamoja na Malori na ofisi ya Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani imetoa wiki tatu ya ukaguzi wa hiari nje ya hapo zoezi la kukamata litaanza. Amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha magari yote yanakuwa katika hali ya ubora na ambaye gari lake halitakaguliwa hata patiwa stika. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  au ukurasa P5Tanzania Limited

VIWANDA VYA MWATEX NA KEKO VIMEPEWA SIKU 14 VIZALISHE BIDHAA

Image
Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa kiwanda cha nguo cha Mwatex cha jijini Mwanza na cha dawa cha Keko jijini Dar es Salaam kuanza uendeshaji wa kiuzalishaji. Amesema kinyume cha hilo,viwanda hivyo vitataifishwa na kurejeshwa kwenye umiliki wa umma. Rais Magufuli amesema hayo jana alipozungumza na wananchi baada ya kuzindua kiwanda cha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical eneo la Buhongwa jijini Mwanza. Amesema Serikali imechoka kusikia kauli na maelezo ya “tuko kwenye mchakato” zinazotolewa kama kinga kwa viwanda visivyofanya kazi kwa kiwango kinachostahili. Rais ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa kiwanda cha Mwatex kinafanya kazi kwa asilimia 20 ya uwezo wake wa uzalishaji. Akizungumzia ujenzi wa kiwanda cha dawa,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema utawezesha mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa bei nafuu. Mwalimu amesema katika utekelezaji wa Tanzania ya viwanda,wi...

MH.ZITTO AMEPEWA DHAMANA

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam. Mwanasheria wa Zitto Kabwe amesema mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015. Mwanasheria amesema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama watakwenda mahakamani. Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa mahakamani ili kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo. Mbali na hilo kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka wanachama pamo...

MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA AMERUHUSU AJIRA ZA MUDA

Image
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ameagiza kuajiriwa kwa baadhi ya maafisa kata wa muda katika baadhi ya Kata. Amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda alipokuwa akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Waheshimiwa madiwani kuhusu tatizo hilo. Katika hatua nyingine amezitaja baadhi ya sababu zilizopelekea upungufu wa watendaji hao kuwa ni baadhi yao kukumbwa na sakata la watumishi wenye vyeti feki. Wiki iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga alitoa agizo kwa vijiji na mitaa kuajiri watumishi wa muda wakati wakisubiri serikali kuu kutangaza ajira. Baraza la Madiwani limeendelea jana ambapo Madiwani wamewasilisha mapendekezo mbalimbali ya utekelezwaji wa bajeti katika kata zao. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited