TIMU YA CCBRT SASA NI MKOANI KIGOMA
Akiongea na timu hiyo mkuu wa mkoa wa
Kigoma Bregedia mstaafu Emanueli Maganga ameeleza kufurahishwa kwake na juhudi
zinazofanywa na CCBRT na kubariki ujio wa timu hiyo kwani utasaidia katika
kueneza elimu juu ya ugonjwa huo kwa wakazi wa kigoma.
Kwa upande wake meneja wa mradi wa
fistula kutoka hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es salaam Bwana
Clement Ndahana amesema kuwa kwa kila mwaka zaidi ya akina mama 3000 nchini
hupata ugonjwa wa fistula lakini akina mama 1400 ndio ambao hupata matibabu ya
ugonjwa huo.
Mara baada ya salamu mkoani humo timu
hiyo ya uhamasishaji imeelekea wilayani uvinza kijiji cha Kalia kilichopo
mwambao wa ziwa Tanganyika ambako wataanza
na uhamasishaji wa matibabu ya ugonjwa wa fistula mkoni humo.
Chanzo:Isaac
Isaac,Mhariri-Issack Gerald
Comments