VYOMBO VYA USAFIRI KUFANYIWA UKAGUZI
Wamiliki na madereva wa vyombo vya moto Mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinafanyiwa ukaguzi.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya
usalama Barabarani Mkoani Katavi Nassoro Alphi ambapo amesema zoezi hilo
linafanyika nchi nzima na litadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amesema kuwa kwa mkoa wa katavi wameanza na magari
ya abiria pamoja na Malori na ofisi ya Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani
imetoa wiki tatu ya ukaguzi wa hiari nje ya hapo zoezi la kukamata litaanza.
Amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha
magari yote yanakuwa katika hali ya ubora na ambaye gari lake halitakaguliwa
hata patiwa stika.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments