RAIS MAGUFULI AMETEUA GAVANA MPYA WA BENKI KUU YA TANZANIA(BOT) PIA ANGALIA ORODHA YA WAJUMBE WALIOPATA TUZO SUALA LA MAKINIKIA
Na.Issack Gerald Prof.Frorens Luoga Gavana Mpya BOT Rais John Magufuli amemteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kuchukua nafasi ya Profesa Benno Ndullu anayemaliza muda wake. Rais Magufuli ametangaza uteuzi huo leo akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kutoa vyeti kwa kamati zilizohusika na ripoti za madini nchini. Akizungumza baada ya kutoa vyeti hivyo amesema atamteua gavana kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashauriano kuhusu madini kutokana na kuridhishwa na kazi yao. Gavana Beno Ndullu,ambaye amekuwa Gavana wa BOT tangu 2008 anamaliza muda wake ifikapo mwezi Januari mwakani. Huo ni uteuzi wa pili kwa Profesa Luoga,kwani Julai 11 mwaka huu Rais Magufuli alimteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA). Profesa Luoga alichukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa. ORODHA WALIOTUNUKIWA VYETI 1.Jobu Yusto Ndugai(Spika wa Bu...