WAKAZI WAANGUA KILIO BOMOABOMOA MKOANI TABORA
Serikali Mkoani Tabora Kwa Kushirikiana Na Halmashauri Ya
Manispaa Ya Tabora Imeendesha Zoezi La Bomoa Bomoa Kwenye Nyumba Zaidi Ya
60 Zilizojengwa Kinyume Cha Sheria Katika Maeneo Ya Shule Ya Sekondari Tabora
Wasichana.
Zoezi hilo limeibua
Vilio,Majonzi Na Simanzi Miongoni Mwa Wananchi Waliobomolewa Nyumba Zao Huku
Wengine Wakipoteza Fahamu Katika Kata Ya Ng’ambo Mjini Tabora.
Zoezi La
Kubomoa Nyumba Hizo Limefanyika Chini Ya Ulinzi Mkali Wa Askari Polisi Na
askari mgambo.
Wakizungumza
Kwa Majonzi Baadhi Ya Wanachi wameiomba serikali kuwatizama kwa jicho la
huruma.
Baadhi ya maafisa Wa Serikali ambao wamesimamia zoezi La Kubomoa
Nyumba Wamewatahadharisha Wananchi Kuacha Tabia Ya Kujenga Bila Kupata Kibali.
Zaidi ya kaya sitini hazina makazi huku wananchi wakiwa hawajui
hatima yao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments