WAJUMBE SAKATA LA MAKINIKIA KUIBUKA NA TUZO LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli leo anatarajia kuwatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya
uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye
kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.
Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano Oktoba
19 mwaka huu na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna
kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika
migodi yake hapa nchini,.
Aidha kutiliana saini huko kumekwenda sambamba na na kulipa Dola
za Marekani Milioni 300 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa
mapato yaliyotokana na biashara hiyo.
Tukio hilo linalotarajiwa kufanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
kuanzia saa 5:00 asubuhi linatarajiwa kurushwa moja kwa moja na vyombo vya
habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali.
Comments