POLISI,JAJI MKUU WATOA ONYO MGOMO WA MAWAKILI HAPA NCHINI-Agosti 28,2017
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini,wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS),kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi,vinavyochunguza tukio la mlipuko,uliotokea kwenye ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.