POLISI WAWEKA WAZI MAJIBU YA UCHUNGUZI OFISI ZA MAWAKILI IMMMA KULIPULIWA-Agosti 28,2017
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo limesema kuwa
uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi
yao walifika katika ofisi za Mawakili wa IMMMA Advocates wakiwa katika magari
mawili na kujifanya ni maaskari na kuwarubuni walinzi na kuondoka nao katika
gari mojawapo kabla ya kulipua jengo hilo.
Walinzi hao wanadaiwa kukutwa baadaye maeneo ya Kawe wakiwa
hawajitambui.
Imedaiwa kuwa kundi lililobaki liliingia katika ofisi hizo hilo
na kuweka vilipuzi vilivyotengenezwa kienyeji, ambavyo vililipuka muda mfupi
baada ya watu hao kuondoka eneo hilo na kusababisha uharibifu wa wa mali na
jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.
Jeshi hilo limesema kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina
ili kubaini watu waliofanya tukio hilo na kujua dhamira yao ili wafikishwe
katika vyombo vya sheria kwani wajibu wa jeshi la polisi ni kulinda raia na
mali zao na kamwe haliwezi kuhujumu maisha ya watu na mali za wananchi
Aidha, jeshi hilo limewaomba waathirika wa tukio hilo na
wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na
upelelezi wa tukio hilo.
Comments