Posts

Showing posts from March 13, 2018

DC TANGAYIKA AKAZA MWENDO DHIDI YA WAHARIFU

Image
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinaendelea kuwasaka na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama wa raia na mali zao ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Muhando ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kuhusu utekelezaji wa agizo lake alilolitoa hivi karibuni akiwataka wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha ambapo amesema silaha tatu zimekamatwa. Aidha pamoja na mambo mengine Mhando amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kupambana na uharifu unaojitokeza huku akiwataka wanaomiliki silaha bila kibali halali kuendelea kuzisalimisha ili kuepuka mkono wa sheria. Wakazi wilayani Tanganyika wanataja miongoni mwa matukio yanayotokea mbali na mauaji kuwa ni uporaji wa mali za raia nyakati za usiku tangu kuanza mwaka 2018. Januari 22 mwaka huu,mkuu wa Wilaya Salehe Mhando akiwa ziarani kata ya Kasekese alitoa agizo kwa wanaomiliki silaha kinyume na sh...