DC TANGAYIKA AKAZA MWENDO DHIDI YA WAHARIFU
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi Salehe Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo
vinaendelea kuwasaka na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama
wa raia na mali zao ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Muhando ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza kuhusu utekelezaji wa agizo lake alilolitoa hivi karibuni akiwataka
wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha ambapo amesema silaha tatu
zimekamatwa.
Aidha pamoja na mambo mengine Mhando
amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili
kupambana na uharifu unaojitokeza huku akiwataka wanaomiliki silaha bila kibali
halali kuendelea kuzisalimisha ili kuepuka mkono wa sheria.
Wakazi wilayani Tanganyika wanataja
miongoni mwa matukio yanayotokea mbali na mauaji kuwa ni uporaji wa mali za
raia nyakati za usiku tangu kuanza mwaka 2018.
Januari 22 mwaka huu,mkuu wa Wilaya
Salehe Mhando akiwa ziarani kata ya Kasekese alitoa agizo kwa wanaomiliki
silaha kinyume na sheria kuzisalmisha kabla ya msako kuanza baada ya Februari 4
mwaka huu.
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments