RAIS MAGUFULI AMEKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UGANDA
Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na Watanzania waishio nchini Uganda katika Mji wa Masaka na kuwahakikishia kuwa hatua zilizoanza kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta mabadiliko zimeanza kuzaa matunda. Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Mawaziri na viongozi wakuu wa taasisi za Serikali ametaja baadhi ya matokeo hayo kuwa ni kusimamia vizuri uchumi unaokuwa kwa wastani wa asilimia 7, kudhibiti mfumuko wa bei hadi asilimia 5.1, kuokoa Shilingi Bilioni 238 walizokuwa wanalipwa watumishi hewa kwa mwaka na kuondoa watumishi wenye vyeti feki waliokuwa wakilipwa Shilingi Bilioni 142 kwa mwaka. Matokeo mengine ni kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Shilingi Bilioni 850 hadi wastani wa Shilingi Trilioni 1.2 kupitia Mamlaka ya Mapato ( TRA ), kuanza ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa ( Standard Gauge ) kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma umbali wa kilometa 726 amba...