SUALA LA BOMOABOMOA KATA YA SITALIKE LIMEFIKA BUNGENI
Na.Issack Gerald
Wizara ya Mali asili na Utalii imesema haina
mpango wa kuruhusu shughuli za kilimo katika Kijiji cha Matandalani na Igongwe
kata ya Stalike iliyopo mkoani Katavi.
Kauli hiyo imetolewa na naibu Waziri wa Mali
asili na Utalii Japhet Hasunga alipo kuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la
Nsimbo mkoa wa Katavi Richad Mbogo ambaye amehoji kwanini maeneo hayo yasi
idhinishwe kisheria kwa shughuri za kibinadam.
Akijibu swali hilo amesema
serikali imetenga maeneo mengine kwa ajili ya wakazi walio ondolewa katika
maeneo hayo yanayotajwa kuwa hifadhi za misitu.
Katika
hatua nyingine amefafanua uwepo wa mpango wa kuyapitia upya maeneo hayo ili
kuona uwezekano wa kubadilisha matumizi pale itakapo onyesha ulazima huo.
Mara kwa
mara mamia ya wakazi mkoani Katavi wamekuwa wakiondolewa kinguvu katika maeneo
mbali mbali ya vitongoji na Vijiji kwa madai ya kuvamia misitu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments