MWANAFUNZI ALIYEPOTEA TANZANIA APATIKANA AKIWA HAJITAMBUI
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa kusini magharibi mwa nchi hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akiongea na waandishi wa habari kuelezea tukio la kupatikana kwa Mwananchuo Abdul Nondo Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha polisi kilichoko karibu. Mahojiano yake katika kituo cha Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye kupiga simu kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe,baba mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kutekwa k...