MFAHAMU RAIS JACOB ZUMA AMBAYE AMEJIUZULU URAIS
Jacob Gedleyihlekisa Zuma alizaliwa Aprili 12, 1942 . Ni Rais wa Afrika Kusini tangu 2009.Alikuwa makamu wa rais chini ya Thabo Mbeki kati ya 1999 na 2005.Tangu Desemba 2007 ni mwenyekiti wa chama tawala cha ANC . KIJANA NA MWANAHARAKATI WA ANC Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini katika eneo la Kwa Zulu-Natal .Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya apartheid (ubaguzi wa rangi wa kisheria). Mwaka 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko Robben Island pamoja na Nelson Mandela ambapo baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko Msumbiji na Zambia na aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC. KUPANDA NGAZI KATIKA AFRIKA KUSINI HURU Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika Kusini mwaka 1990,Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha ...