BARAZA LA MADIWANI LACHARUKA UPIGAJI CHAPA MIFUGO CHINI YA KIWANGO
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani
Singida limewajia juu wataalamu wake kwa kutotekeleza kwa weledi upigaji chapa
mifugo na kuwatishia kuwa watalamika kwenda kurudia zoezi hilo kwa gharama zao
iwapo alama zinazowekwa zitafutika baada ya muda mfupi.
Katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya
ya Iramba kilichofanyika Mjini Kiomboi, ajenda iliyochukua uzito mkubwa ni juu
ya kufutika kwa alama zilizowekwa kwenye upigaji chapa mifugo na kuchelewa kwa
malipo ya wananchi walioshiriki kusaidia utekelezaji wa zoezi hilo.
Afisa mifugo Wilaya ya Iramba Andrew Manyerere anasema kuwa
ingawa zoezi hilo lilitekelezwa kwa kuzingatia sheria lakini kwa mifugo ambayo
alama zake zimefutika watarudia bila malipo.
Hata hivyo uamuzi wa baraza la madiwani wa uliotolewa na Mwenyekiti
wake Simion Tyosela ni kwa wataalamu kufanyakazi hiyo kwa weledi vinginevyo
watarudia zoezi hilo kwa gharama zao.
Zaidi ya shilingi milioni 16 zimetumika kuwalipa wanachi
waliosaidia zoezi hilo ambapo jumla ya ng’ombe 190,000 wamepigwa chapa katika
kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments