GESI YA HELIUM YA FUTI ZA UJAZO BILIONI 98.9 YAGUNDULIWA MKOANI RUKWA
Kampuni ya uchunguzi na utafiti wa madini Helium One, ambayo kwa sasa inafanya utafiti wa gesi ya heliamu mkoa wa Rukwa imegundua kuwapo kwa futi za ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo katika maeneo iliyokwishafanyia uchunguzi. Hayo yalielezwa katika warsha ya siku moja iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kuratibiwa na Idara ya Jiolojia ya chuo hicho Helium One na Chuo Kikuu cha Oxford. Akizungumza katika warsha hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Helium One,Thomas Abraham-James alisema kampuni yao imetafuta leseni 23 za uchunguzi na kwamba nyingine tatu zimeombwa. Alisema leseni hizo zote zinamilikiwa na kampuni hiyo kwa asilimia 100 na kwamba ina haki za kipekee za gesi hiyo ya heliamu . Pamoja na kutoa taarifa hiyo,alisema lengo la kuwa na warsha ni kuwaita wataalamu na wadau mbalimbali wa hapa nchini na kimataifa kubadilishana uzoefu na taarifa zilizopo kuhusu gesi hiyo na kuangalia fursa zinazoambatana na uwapo wa gesi hiyo katika harakati za kitaifa za kuwa na taifa...