AJALI MKOANI KATAVI
Watu wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea katika eneo la mpanda hotel barabara iendayo Kigoma baada ya gari na pikipiki kugongana.
Kamanda wa usalama barabarani mkoani Katavi
John Mfinanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa
pikipiki kutaka kulipita gari na ndio akasababisha ajali.
Kwa upande wao mashuhuda wa ajali
hiyo wamemtuhmu dereva wa gari ambaye ni
askari polisi kuwa katika mwendo mkali hali iliyofanya ashindwe kumudu usafiri
huo na kusababisha kutokea kwa ajali hiyo.
Mfinanga amesema majeruhi hao
wanapatiwa matibabu katika hospitali ya manispaa ya mpanda.
Mwaka uliopita ajali kama hiyo
ilitokea ikihusisha dereva wa pikipiki na gari na kusababisha majeruhi kwa
waliogongana.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments