RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia
salamu za rambirambi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma kufuatia
kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe.Robert Kisanga
kilichotokea jana.
Rais Dkt.John Magufuli |
Kwa
mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULu Gerson
Msigwa
Marehemu
amefariki jana katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam.
Katika
salamu hizo Mhe.Rais Magufuli amesema Jaji Mstaafu Robert Kisanga atakumbukwa
kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa wakati wote wa utumishi wake uliojaa
umakini,uchapakazi,uzalendo na ushirikiano.
Aidha
Mhe.Rais Magufuli amewaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira,uvumilivu na
ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea Marehemu Jaji
Mstaafu Kisanga apumzishwe mahali pema peponi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments