MKUU WA WILAYA AAMURU ALIYEMKASHIFU RAIS MAGUFULI ATUPWE NDANI MASAA 48
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara,Chelestino Mofuga amemuagiza Mkuu wa Polisi wilayani humo kumkamata Eliud Petro (50) akituhumiwa kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais.
Mofuga
ametoa kauli hiyo jana Jumanne Januari 23,2018 akitaka Petro akamatwe na
kuwekwa ndani kwa saa 48 na baadaye kufikishwa mahakamani.
Amesema
mtuhumiwa alitumia lugha hiyo baada ya kukamatwa na polisi kwa kosa la kuvamia
eneo la Shule ya Msingi Endamasak na kulima.
Mofuga
amesema wakati polisi wakiendelea kuwakamata wenzake wanne, Petro alitamka kuwa
Rais John Magufuli naye ni mtuhumiwa bila
kufafanua anatuhumiwa kwa kosa gani.
Amebainisha
kuwa Petro na wenzake walikamatwa kwa kosa la kuvamia na kulima eneo la shule
hiyo.
Amewataja
watuhumiwa wengine kuwa ni Yohana Baida, Boay Nonash,Paulo Gutii na Martin
Joseph.
Mofuga
amesema kwa mamlaka aliyonayo amemuagiza mkuu wa polisi wa wilaya kumweka
rumande kwa saa 48 mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments