RAIS ASHTUSHWA NA KIFO ATUMA SALAAMU ZA RAMBIRAMBI
Marehemu Jumanne Ntambi |
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Jumanne Ntambi na wachezaji wa Mwadui kwa kuondokewa na kocha wao usiku wa kuamkia leo huku akiwataka wafiwa wawe na moyo wa subira
Rais Karia amesema hayo katika salamu
zake zilizotolewa rasmi na Shirikisho hilo huku akisema ameshtushwa kupata
taarifa hizo kwani marehemu Ntambi alikuwa na mchango mkubwa katika soka la
Tanzania.
Enzi za uhai wake Jumanne Ntambi
aliwahi kufundisha timu za Kahama United ya Shinyanga, Mlale JKT ya Ruvuma,
Panone ya Kilimanjaro,timu ya mkoa wa Shinyanga Igembe Nsabo na mpaka mauti
yanamkuta alikuwa akiifundisha Mwadui ya Shinyanga akiwa kocha msaidizi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments