MWANAKWAYA MKOANI RUKWA AFARIKI BAADA YA KUTOA SADAKA
Mwanakwaya wa kwaya ya
Mtakatifu Secilia,Kigango cha Muze Parokia ya Zimba,Jimbo Katoliki Sumbawanga,Flora
Nandi (25) ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya
shukrani akiwa kanisani.
Tukio hilo limetokea siku
ya Jumapili saa nne za asubuhi wakati wa ibada ya kwanza,kwaya ya
Mtakatifu Secilia ikimsifu Mungu katika ibada hiyo.
Akizungumzia tukio hilo,mwalimu
wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo,Katekista Philipo Lupadasi amesema
wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya shukrani na
kuendelea kuimba ghafla alianguka chini hali iliyozua mshtuko na kusababisha
ibada kusimama kwa muda.
Amesema baada ya kufikishwa
katika zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya ambao baada ya kumfanyia
uchunguzi walibaini kuwa alikuwa ameshafariki dunia.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments