CHANGAMOTO SKIMU YA UMWAGILIAJI RUKWA, MKUU WA MKOA ATOA AGIZO KALI KWA WAFUGAJI WA MIFUGO
Na.Issack Gerald MRADI wa skimu ya umwagiliaji ya Ng'ongo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa,unazidi kupungua uwezo wa kuzalisha mazao siku hadi siku kutokana na ukosefu wa maji pamoja na wafugaji wanaofuchungia mifugo katika eneo hilo. Akizungungumza jana mbele ya mkuu wa mkoa wa Rukwa,mwenyekiti wa mradi wa scheme ya umwagiliaji ya Ng'ongo Justine Amon alisema kwa kipindi cha mwaka 2015 /2016 wakulima walilima hekta 128 na kufanikiwa kuzalisha tani 460.8 za mahindi. Alisema katika msimu wa mwaka 2016/2017 katika hekta hizo 128 uzalidhaji umeshuka hadi kufikia tani 358.4 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo haribifu wa mazingira pamoja na wafugaji kuchungia ndani ya eneo la uzalishaji. Amon alisema eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 630 lakini zinazolimwa ni hizo 128 tu kwa kuwa ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 3,000 haujakamilika kwa muda mrefu sasa. Mpaka sasa mfereji uliokalimilika unaurefu wa mita 1,725 ambao ndiyo unatumika katika umwagiliaji wa h...