MENEJA MPANDA RADIO FM ATOA NENO KWA WANASALAAM,LEO KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI
Na.Issack Gerald Wadau wa salaamu kupitia vyombo vya habari Mkoani Katavi,wameaswa kushiriki kwa kiasi kikubwa kuibua masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuibua matukio yanayoiathiri jamii kama ukatiri. Baadhi ya watuma Salaamu Mkoani Katavi wakiwa katika kikao na watumishi Mpanda Radio katika Ukumbi wa Mpanda Radio(PICHA NA.Issack Gerald) Wito huo umetolewa leo na Meneja wa kituo cha Mpanda Radio Bw. Revocatus Msafiri,wakati akizungumza na viongozi wa vikundi vya wanasalaamu kuanzia ngazi ya kata hadi Mkoa kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa studio ya Mpanda Radio. Katika hatua nyingine, Bw.Msafiri amesema bonanza la leo la mchezo wa mpira wa miguu baina ya watumishi Mpanda Radio na watuma salaamu Mkoani Katavi linalenga kupanua wigo wa kufahamiana na kuongeza mahusiano yenye tija kwa jamii. Baadhi ya wafanyakazi wa Mpanda Radio Kwa upande wao watuma salaamu mbali na kuipongeza Mpanda Radio kwa matangazo yanayozingatia mahitaji ya jamii,pia wamek...