MENEJA MPANDA RADIO FM ATOA NENO KWA WANASALAAM,LEO KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI
Na.Issack
Gerald
Wadau wa salaamu kupitia vyombo
vya habari Mkoani Katavi,wameaswa kushiriki kwa kiasi kikubwa kuibua masuala
mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuibua matukio yanayoiathiri jamii kama ukatiri.
Baadhi ya watuma Salaamu Mkoani Katavi wakiwa katika kikao na watumishi Mpanda Radio katika Ukumbi wa Mpanda Radio(PICHA NA.Issack Gerald) |
Wito huo umetolewa leo na
Meneja wa kituo cha Mpanda Radio Bw. Revocatus Msafiri,wakati akizungumza na
viongozi wa vikundi vya wanasalaamu kuanzia ngazi ya kata hadi Mkoa kikao
ambacho kimefanyika katika ukumbi wa studio ya Mpanda Radio.
Katika hatua nyingine, Bw.Msafiri
amesema bonanza la leo la mchezo wa mpira wa miguu baina ya watumishi Mpanda
Radio na watuma salaamu Mkoani Katavi linalenga kupanua wigo wa kufahamiana na
kuongeza mahusiano yenye tija kwa jamii.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mpanda Radio |
Kwa upande wao watuma salaamu
mbali na kuipongeza Mpanda Radio kwa matangazo yanayozingatia mahitaji ya
jamii,pia wamekiomba chombo hiki cha habari kuwafikia zaidi wananchi waishio
vijijini kutokana na vyombo vya habari kutofika mara kwa mara.
Kituo cha Mpanda Radio ambacho ni cha Kijamii
kilianza kurusha matangazo yake mwaka 2013 kikiwa na lengo la
kuelimisha,kuhabarisha na kuburudisha jamii na kilizinduliwa na mwenge wa uhuru
Julai 17 mwaka 2017.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments