IGP SIRRO AWAHAKIKISHIA USALAMA WATANZANIA WOTE KIPINDI CHA PASAKA
Amesema Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini. IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ili kutoa salaamu za pasaka kwa watanzania ambapo amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini. Aidha amesema jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia. Katika hatua nyingine amesema jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka. Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia,fukwe,...