RIPOTI YA DAKTARI KUHUSU WALIOKUFA KWA SUMU YA UYOGA KATAVI HII HAPA
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Dkt. Theopister Elisa amesema uchunguzi wa kitabibu unaonesha mwanamke
Mariana Gerald Sanane(47) mkazi wa kijiji cha Sitalike Wilayani Mpanda
aliyefariki duniani baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na sumu aliathiriwa
katika ini.
Dkt.Theopister Elisa ameeleza hayo
wakati akizungumza na vyombo vya habari kueleza walichokibanini kwa mwanamke
huyo baada ya kufariki kwa kula uyoga ambao unadaiwa kuchumwa kutoka zizi la
ng’ombe baada ya uyoga huo kumwagiwa dawa ya kupulizia ng’ombe.
Aidha Dkt.Elisa amesema waathiriwa wa
sumu hiyo walicheleweshwa kufikishwa katika vituo vya huduma za afya hali
iliyosababisha mathara makubwa kujitokeza mwilini mpaka kusababisha mauti baada
ya idi kuathirika.
Machi 25 mwaka huu Frenki Mayaga na
Erizabeth George wakazi kijiji cha Sitalike wakiwa wa familia moja,walifariki
dunia baada ya kula uyoga huo wenye sumu na hivyo kufikisha idadi ya watu
watatu waliofariki dunia wote wakitoka katika familia hiyo.
Hata hivyo Dkt.Elisa amesema mwanamke
mmoja mwenye umri wa miaka 60 aliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji cha
Sitalike Bw.Christopher Anjero,tukio hilo la kusikitisha halijatokea katika
kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANI.BLOGSPOT.COM
Comments