DKT.SHEIN AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo amewaapisha viongozi aliowateua
hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Viongozi walioapishwa na Rais Dk.Shein
katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye
ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee, Wanawake na Watoto
na Abdalla Hassan Mitawi ambaye ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamo wa Pili wa Rais.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,Spika wa Baraza
la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid,Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri.
Viongozi wengine waliohudhuria hafla
hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih,Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Khamis Haji,Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi
wengine wa Serikali.
Kwa upande wa walioapishwa waliahidi
kutekeleza majukumu yao kwa ushirikiano wa pamoja kati yao na viongozi wengine
wote wa Serikali wakiwemo wale wa Wizara zao pamoja na Ofisi watakazoziongoza.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments