Posts

Showing posts from November 16, 2017

NDEGE IMEANGUKA ARUSHA NA KUUA WATU 11

Image
Shirika la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali ya ndege iliyotokea jana  asubuhi limesema watu wote 11 waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki dunia. Coastal wameeleza kuwa,ndege yao Cessna Caravan ilipata ajali majira ya saa 5 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki katika eneo la Empakaai,Ngorongoro ikiwa na rubani mmoja na abiria 11 wakati ikiwa safarini kuelekea Serengeti. Shirika hilo limesema majina ya waliofariki katika ajali hiyo bado hayajawekwa wazi wakisubiria kuwajulisha ndugu zao. Mkurugenzi Mkuu wa Coastal,Julian Edmunds amesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana, na kwamba mara kadhaa amekuwa akisafiri na ndege za shirikia hilo na hivyo anaimani na marubani pamoja na ndege zao. Aidha,ameeleza kuwa kwa niaba ya shirikia hilo na wafanyakazi wake, watafanya kila litakalowezekana ndani ya uwezo wao kusaidia katika uchunguzi wa ajali hiyo kwani hakuna kitu cha umuhimu kwao zaidi ya usalama wa abiria. Kwa sasa wameeleza kwamb...

SERIKALI IMEZIRUHUSU HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI

Image
Na.Issack Gerald Serikali imetoa ruksa kwa Halmashauri nchini kuajiri maafisa watendaji wa kata pale inapoona kunaupungufu. Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa alipokuwa akijibu maswali yaliyo ulizwa na wabunge mapema leo. Waziri Mkuu amefafanua kuwa serikali inatambua uwepo wa upungufu wa watumishi wa kada mbali mbali hali iliyosababishwa na zoezi la uhakiki wa watumishi hewa ilikiwemo vyeti feki. Halmashauri nyingi nchini Tanzania zimekumbwa na tatizo hilo la uhaba wa watumishi jambo linalotajwa kuwa kikwazo katika mstakabali wa maendeleo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKULIMA WILAYANI TANGANYIKA WAMEALALAMIKIA GHARAMA ZA PEMBEJEO ZA KILIMO

Image
Na.Issack Gerald Wakulima kata ya Mpanda ndogo wilayani Tanganyika mkoani Katavi wameiomba serikali kupunguza gharama za pembejeo za ruzuku. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wamesema bei wananyonunua pembejeo kwa sasa ni kubwa hali inayowakwamisha kufikia malengo yao katika kilimo. Wamesema serikali iweke utaratibu utakaowasaidia wakulima kupata pembejeo kama mbegu na mbolea ambazo watazinunua kwa bei nafuu. Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais DK John Pombe Magufuli inahimiza Tanzania ya viwanda ilikufikia, mpango huu mikakati inahitajika katika kuwainua wakulima nchi Tanzania Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MKOA WA KATAVI KUPATIWA MADAKTARI BINGWA

Image
Na.Issack Gerald Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa itakayopatiwa madaktari bingwa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wangonjwa. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu waziri wizara ya Afya Dk Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa viti maalumu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA Roda Kunchela aliyetaka kujua lini serikali italimaliza tatizo hilo. Akijibu swali hilo amesema tayari serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kulikabili suala hilo kwa mkoa wa Katavi na maeneo mengine. Licha ya hayo serikali ya mkoa wa Katavi iko mbioni kuanza ujenzi wa hosipitali ya rufaaa itakayo toa huduma kwa mkoa mzima ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 1 ilikwishapatikana kwa ajili kuanza ujenzi wa Hospitali hiyo. Mwezi Julai mwaka huu,Waziri wa afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia ,wazee na watoto mh.Ummy Mwalimu aliahidi kuleta pesa mkoani Katavi ili kuongeza nguvu katika ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Katavi. Habari zaidi ni P...

SERIKALI KUTOA KAULI YA MAAMUZI KUHUSU VIJIJI VINAVYODAIWA KUWA SEHEMU YA HIFADHI.

Image
Na.Issack Gerald Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali inatarajia kutoa maamuzi baada ya kubaini vijiji vyote nchini vinavyodaiwa kuwa vipo katika maeneo ya hifadhi hapa nchini. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mh.John Peter Kadutu Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu Mkoani Tabora,aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu migogoro baina ya hifadhi na wananchi ambapo baadhi wananchi wanazuiliwa na kufukuzwa licha ya baadhi ya vijiji kusajiliwa na serikali. Aidha Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwaacha wataalumu wa ardhi wanaobainisha mipaka kati ya hifadhi na vijiji wafanye kazi yao ya kuweka alama kama kawaida. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hivi karibuni alitoa agizo kwa wizara ya Maliasili na utalii kupitia na kuweka mipaka na alama maeneo yote yenye migogoro ya ardhi na wanatakiwa wawe wamekamilisha zoezi hilo mpaka kufikia Desemba 30 mwaka huu ili serikali ichukue maamuzi. Mkoa wa Kata...