SERIKALI KUTOA KAULI YA MAAMUZI KUHUSU VIJIJI VINAVYODAIWA KUWA SEHEMU YA HIFADHI.
Na.Issack Gerald
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali inatarajia kutoa maamuzi baada ya
kubaini vijiji vyote nchini vinavyodaiwa kuwa vipo katika maeneo ya hifadhi
hapa nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mh.John Peter Kadutu Mbunge wa Jimbo la
Ulyankulu Mkoani Tabora,aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu migogoro baina ya hifadhi na wananchi ambapo baadhi
wananchi wanazuiliwa na kufukuzwa licha ya baadhi ya vijiji kusajiliwa na
serikali.
Aidha
Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwaacha wataalumu wa ardhi wanaobainisha mipaka
kati ya hifadhi na vijiji wafanye kazi yao ya kuweka alama kama kawaida.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema hivi karibuni alitoa agizo kwa wizara ya Maliasili
na utalii kupitia na kuweka mipaka na alama maeneo yote yenye migogoro ya ardhi
na wanatakiwa wawe wamekamilisha zoezi hilo mpaka kufikia Desemba 30 mwaka huu
ili serikali ichukue maamuzi.
Mkoa wa
Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye migogoro ya ardhi baina ya maeneo ya hifadhi
na makazi ya watu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments