SERIKALI KUSAMBAZA MAJI MAENEO MBALIMBALI MKOANI KATAVI KUTOKEA ZIWA TANGANYIKA
Na.Issack Gerald
Serikali imesema kuanzia mwaka wa
fedha 2018/2019 wanatarajia kuweka fedha katika mradi wa maji Ziwani
Tanganyika,ili kuwezesha kuvuta maji kutoka Ziwa Tanganyika na kusambazwa
katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni
Dodoma na Waziri wa maji na umwagiliaji Issack Kamwelwe,wakati akijibu swali la
mbunge wa Mpanda vijijini Suleimani Kakoso aliyetaka
kujua mpango wa serikali kuvuta maji kutoka Ziwa Tanganyika hadi Mpanda Mjini.
Waziri
Kamwelwe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Katavi Mkoani Katavi,amesema wizara
imepokea andiko la mradi huo wa kuvuta maji kutoka ziwa Tanganyika na mradi huo
utatekelezwa kama sehemu ya kumaliza tatizo la maji Mkoani Katavi.
Kwa sasa wakazi wa Mpanda wanapata maji kutoka vyanzo kama bwawa la milala na maji ya mseleleko Ikorongo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Kwa sasa wakazi wa Mpanda wanapata maji kutoka vyanzo kama bwawa la milala na maji ya mseleleko Ikorongo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments