JELA SIKU 14,KWA KUMCHANACHANA KWA NYEMBE MTOTO WAKE WA MIAKA 6
Na.Issack Gerald-MPANDA Mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda imemhukumu Bi. Agnes George (30) mkazi wa Kawajense mjini Mpanda kwenda jela kwa siku kumi na nne, baada ya kupatikana na hatia ya kumkatakata kwa nyembe nyuma ya viganja mtoto wake mwenye umri wa miaka sita, akimtuhumu kuiba fedha.