MLELE NAKO MAUJI KAMA MPANDA,MMOJA AUAWA,WAUAJI WATOKOMEA POLISI MSHIKEMSHIKE KUWASAKA WAUAJI
Na.Issack Mlele-Katavi
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Chalya
Kichosha(60) mkazi wa mkazi wa kijiji cha Ibindi alikutwa akiwa ameuawa na watu
wasiojulikana kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani na
shingoni.
Mratibu wa Polisi Mkoani Katavi SSP Focas
Malengo amesem akuwa tukio hilo limetokea Mnamo tarehe 02/01/2016 majira ya saa
sita usiku katika kitongoji cha Ipilito Ibindi kata ya Ibindi Tarafa ya Nsimbo
Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi.
SSP Malengo amesema,siku ya tukio,wauaji
walifika nyumbani kwa marehemu majira ya usiku na kuvunja mlango kisha kuingia
ndani na kisha kuanza kumshambulia kwa
kumkata sehemu za kichwani na shingoni hadi kupelekea umauti wake.
Chanzo cha mauaji hayo bado kujulikana.
aidha, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wanakijiji cha ibindi linafanya
msako ili kuweza kuwabaini wahusika wa tukio hilo.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi
anatoa wito kwa wananchi kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mikononi
kwa kutoa uhali wa binadamu wenzao badala yake wafate taratibu za kisheria
katika kuwasilisha jambo au malalamiko dhidi yao katika vyombo vya kisheria ili
kushughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Aidha, anaitaka jamii iendelee
kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili
kufanikisha operesheni na misako ya kuwabaini na kuwakamata wote wa mauaji haya
ili kuendelea kutokomeza vitendo vya namna hii ndani ya jamii
Asante kwa kuendelea
kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
Chanzo
cha habari :Ofisi ya mawasiliano ya Waziri
Comments