JELA SIKU 14,KWA KUMCHANACHANA KWA NYEMBE MTOTO WAKE WA MIAKA 6
Na.Issack
Gerald-MPANDA
Mahakama
ya Mwanzo mjini Mpanda imemhukumu Bi. Agnes George (30) mkazi wa Kawajense
mjini Mpanda kwenda jela kwa siku kumi na nne, baada ya kupatikana na hatia ya kumkatakata
kwa nyembe nyuma ya viganja mtoto wake mwenye umri wa miaka sita, akimtuhumu
kuiba fedha.
Akitoa
ushahidi mahakama hapo, askari polisi wa kata, WP 3207 Copral Regina, ameiambia
mahakama kuwa tukio hili lilitokea tarehe 25 Mwezi Novemba mwaka 2015 majira ya
saa 3 asubuhi, alipigiwa simu na mwenyekiti wa mtaa wa Kawajense Bw. William
Richard maarufu maka Jumapili akimtaarifu kuwa mtaani kwake kuna mama
amekatakata mwanaye kwa wembe na alienda kwenye eneo la tukio la kumkuta
mtuhumiwa akiwa amewekwa chini ya ulinzi na mama wneye nyumba, pamoja na akina
mama wengine watano.
Amesema
alimweka chini ya ulinzi na alishuhudia mtoto aliyejeruhiwa akiwa anatokwa na
damu nyuma ya viganja vya mikono yake huku nyama nyeupe ikiwa inaonekana.
Mtuhumiwa
alibebwa kwenye bajaji kwa ushirikiano na mwenyekiti wa mtaa, hadi kituo cha
polisi mjini Mpanda kwa hatua zaidi za kisheria.
Copral
Regina ameiambia mahakama hiyo kuwa, baada ya kugundua mtoto aliyejeruhiwa ana
umri mdogo na hawezi kujieleza aliamua kumfungulia Agnes George shtaka la
kujeruhi na hati ya matibabu ilitolewa na mtoto huyo alipelekwa hospitali na
mshtakiwa baada ya kupewa dhamana.
Taratibu
za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa zilifanyika na hatimaye leo amefikishwa
katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda ili kujibu mashtaka yanayomkabili.
Mshtakiwa
amekiri kutenda kosa hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela
na kwamba ushahidi uliotolewa ni wa kweli.
Hakimu Mbembela amesema mshtakiwa ametiwa hatiani
chini ya kifungu cha sheria namba 228 namba 2. Akijitetea mahakamani hapo
Mshitakiwa Agnes George aliiomba mahakama imsamehe kwa kosa la kujeruhi mtoto
wake na kwamba hatarudia tena hata kama mtoto huyo akirudia kuiba fedha
atamfikisha polisi.
Akitoa
hukumu Hakimu Mbembela amesema kulingana na kosa alilotenda mshtakiwa adhabu
yake ni kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, lakini kwa kuwa ni mkosaji wa
mara ya kwanza ingawa mazingira yanaonesha alifanya kosa la unyanyasaji na
hakupaswa kujichukulia sheria mkononi, hivyo mahakama imezingatia maslahi na
umri wa mlalamikaji kwa kuwa bado anamtegemea mshtakiwa.
Mahakam
hiyo imemhukumu kifungo cha siku 14 gerezani ili iwe fundisho kwa watu wenye
tabia za unyanyasaji na kuagiza polisi ishirikiane na maafisa ustawi wa jamii
kuhakikisha mhanga anapata uangalizi na pindi akitoka gerezani itabidi alipe
gharama zitakazotumika kwa matunzo ya mtoto wake wakati akiwa gerezani.
Asante kwa kuendelea kuwa namii,endelea kuhabarika na P5
TANZANI
Comments