TMA WATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA LEO APRILI 13,2018
Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania TMA imesema vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa leo Aprili 13,2018. Katika taarifa ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana Aprili 12,2018 mikoa ambayo inatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa ni Kagera,Geita, Mwanza,Mara, Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora,Katavi,Morogoro, Ruvuma,Dar Es Salaam, Pwani, Tanga Pamoja Na Visiwa Vya Unguja Na Pemba. Aidha TMA imetoa angalizo kwa kusema kuwa Vipindi Vifupi Vya Mvua Kubwa Vinatarajiwa Katika Baadhi Ya Maeneo Ya Mikoa Ya Rukwa, Njombe, Mbeya, Iringa Na Songwe. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com