RC KATAVI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KESHO JUMAMOSI APRILI 14,2018
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral
Mstaafu Raphael Muhuga kesho siku ya Jumamosi Aprili 14,2018 ameitenga kwa ajili
ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Kwa mjibu wa kaimu Katibu Tawala wa
Mkoa wa Katavi,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Mpanda na maeneo mengine ya Mkoa wa Katavi kufika katika viwanja vya Azimio
Mjini Mpanda kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi ili kueleza kero zao.
Muhuga amesema atasikiliza kero za
wananchi wote zinazohusu masuala mbalimbali na kuzipatia majibu papo hapo.
Hii ni mara ya Kwanza kwa Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga,kusikiliza kero za wananchi
katika eneo la wazi linalojumuisha wananchi wote tangu alipoteuliwa mwaka 2016 kuwa
Mkuu wa Mkoa kabla ya hapo amekuwa akisikiliza kero za wananchi Ofisini kwake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments